×

SPOTI HAUSI LIVE: Beach Soccer ni ya Kina Boban, Kaseja

Tazama Kipindi cha Spoti Hausi kupitia Global Tv Online, ambayo imefanya mahojiano na  Mratibu wa Beach Soccer kutoka TFF, Aaron Nyanda ambaye pia ni Ofisa Masoko wa TFF, ambaye amesema walikuwa sahihi kuwaita kikosini wakongwe Haruna Moshi ‘Boban’ na Juma Kaseja kikosini.

Boban na Kaseja anayechezea Kagera Sugar waliitwa na Kocha wa Timu ya Taifa ya Beach Soccer ya Tanzania, John Mwansasu katika kikosi kilichoshiriki michuano maalum ya Copa Dar es Salaam.

Michuano hiyo ilishirikisha timu nyingine za Malawi, Uganda na Zanzibar ambapo Zanzibar ilitwaa ubingwa kwenye viwanja vya Coco Beach jijini Dar es Salaam