×

Mwili wa Mkurugenzi wa Nuru Funeral Services Waagwa na Mamia Dar

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Nuru Funeral Services, Paul Beda Moshi enzi za uhai wake.

MWILI wa Paul Beda Moshi, aliyekuwa Mkurugenzi wa Nuru Funeral Services umeagwa leo na mamia ya waombolezaji, nyumbani kwake Kawe Mlalakuwa na anatarajiwa kusafirishwa kwenda kijijini kwao, Rombo Tarakea, Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.

Moshi alifariki Jumatano ya Januari 3, 2018 na anatarajiwa kuzikwa Jumatatu, Januari 8, 2018 kijijini kwao.

Kwa wasiomjua Paul Beda Moshi, alikua ndiye Mmiliki wa Kampuni ya kukodisha magari ya kusafirisha maiti na alikua dereva pia, ameshasafirisha maiti sana, karibu nchi nzima! Lkn leo hii naye anasafirishwa, kwenye gari alilokuwa akiwasafirisha wenzake Hakika Mungu aliumba kifo ili kutukumbusha kutenda mema hapa duaniani. Ila Paul alisifika sana kwa ukarimu na ucheshi. Pamoja na kufanyabiashara, lkn alisaidia pia wafiwa wengi.

Mwenyezi Mungu Amuangazie Mwanga wa Milele na ampumzishe kwa amani, Ameen!

Gari likiwa limebeba mwili wa marehemu Paul Beda Moshi.
Mwili wa marehemu ukishushwa kutoka kwenye gari.
Mamia ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Kawe Mlalakuwa, Dar.
Mwili wa marehemu ulivyowasili nyumbani kwake.