Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na Shirika la Save the Heart’s Child kutoka nchini Israel na taasisi ya Moyo ya Berlin kutoka nchini Ujerumani, wameendesha uchuguzi maalum kwa watoto wenye matatizo ya moyo ambapo watoto 30 wamechunguza na 20 kati yao, wamegunduliwa kuwa na matatizo yanayohitaji matibabu ya upasuaji wa kitaalamu.
Kwa kushirikiana na wafadhili hao, taasisi hiyo imeanza kuwafanyia upasuaji watoto hao kwa kuwashirikisha madaktari wa Watanzania, ambao wanapatiwa mafunzo ya kitaalamu kwa ajili ya kuendelea kuhudumia watoto wenye matatizo hayo.