MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapa miezi tisa tu (ambapo mwanzoni ilikuwa miezi sita) wafanyabiashara ya magari jijini humo kuhakikisha biashara zao hizo za magari wanazihamishia Kigamboni katika eneo maalum lililoandaliwa na serikali kwa ajili ya bishara hiyo kwa mkoa mzima.
Makonda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wafanyabiashara hiyo mbele ya vyombo vya habari na kueleza kuwa mkakati uliowekwa kurahisisha uhamaji huo.
“Serikali imewatengea maeneo maalum kwa ajiri ya biashara yenu, mfanyabiashara akihitaji eneo hilo hatumlazimishi kulipia hapo hapo, watalipia ndani ya miaka sita huku wakiendelea kufanya biashara,” alisema Makonda.
Aidha ameeleza adhima ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwasaidia wafanyabaishara wa jijini humo kuwaunganisha na wafanyabiashara na serikali za nje ili kukuza zaidi biashara zao na kupata manufaa zaidi.