×

MWIGULU AFANYA MAAMUZI MAGUMU ‘SOKO LA WATUMWA’ WABONGO UGHAIBUNI

Waziri Mwigulu Nchemba.

 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amezuia utoaji wa passport za kusafiria kwa makundi ya watu hadi pale ambapo serikali itakapoweka utaratibu maalum kutokana na kuwepo kwa wimbi la walaghai ambao wamekuwa wakiwachukua vijana Watazania wakafanye kazi nje ya nchi na badala yake wanaishia kwenda kuteswa na kunyanyaswa kama watumwa ughaibuni.

 

Mwigulu ameyasema hayo leo, Alhamisi, Januari 25, 2018 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam;

“Nimezipata taarifa za mateso ya Wananchi wetu wakienda nje ya nchi wanateswa, wananyang’anywa passport zao, wanatumikishwa kikatili, na wengine wanalazimishwa kufanya mambo ambayo hawapendezwi nayo.

 

“Tumewasiliana na wizara zote zinazohusika, tumekubaliana kuchukua hatua kuhusu jambo hili. Nitoe tamko rasmi na kuelekeza kuwa ninasimamisha utoaji wa passport za jumla za makundi ya vijana ambao wamekuwa wakikutana na mikasa hiyo ya kutumikishwa, kunyanyaswa na kuteswa na wengine kuwekwa rehani kwa ishu ya madawa ya kulevya. Tunasimamisha mpaka pale tutakapoweka utaratibu mzuri kati ya serikali na nchi ambako kutakuwa na mahitaji ya watu hawa,” alisema Mwigulu.

VIDEO: MSIKIE MWIGULU AKIFUNGUKA