×

GLOBAL HABARI: JPM, MAMA JANETH WAMPA WASTARA MIL 15 ZA MATIBABU

Rais John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wamechangia Sh. milioni 15 kwa ajili ya matibabu ya msanii Wastara Juma ambazo ziliwazilishwa na Katibu wa Rais, Ngusa Samike nyumbani kwa msanii huyo.

Mbali na Rais Magufuli na Mke wake wasaidizi wa Rais pia wamechangia Shilingi milioni moja na laki tisa kwa ajili ya kusaidia maandalizi ya matibabu ya Wastara ambaye Global Tv imekuwa mstari wa mbele kutangaza habari zake.

Akiwasilisha msaada huo Samike amesema, Rais na Mkewe wameguswa na hali ya Wastara na hivyo kuamua kuchangia matibabu yake.
Akizungumzia hali yake na msaada huo Wastara amemshukuru Rais na Mke wake kwa mchango huo utakaomuwezesha kutibiwa.