
MKAZI wa Morogoro anayefahamika kwa jina la Nasri Jafary, wikiendi hii itakuwa nzuri kwake baada ya kushinda shilingi milioni moja kutokana na kupatia matokeo kupitia Sokabet ambapo aliweka dau la shilingi 200 tu.
Nasri ambaye ana umri wa miaka 24, alipata ushindi huo jana na muda mfupi akatumiwa fedha aliyoshinda kutokana na kupatia matokeo ya michezo aliyotabiri.
Akizungumzia juu ya ushindi huo kutoka Morogoro ambapo ndipo makazi yake yalipo, Nasri alisema kiasi hicho cha fedha kimefika wakati muafaka kwake kwa kuwa alikuwa na uhitaji mkubwa wa fedha na aliamua kushiriki katika Kampuni ya Sokabet kwa kuwa ndiyo yenye kiwango cha chini kuliko kampuni nyingine.
“Unajua kiwango cha chini kabisa kwa Sokabet cha kubet ni shilingi mia mbili, nimekuwa nikishiriki mara kwa mara, hata safari hii niliposhiriki niliweka dau hilo na kuchagua mechi kadhaa, nilikuwa naimani kubwa ya kushinda ila mechi ya Barcelona ndiyo ambayo ilikuwa ikinipa presha.
“Unajua kwa sasa shughuli zangu nazifanyia Tanesco Morogoro, kiukweli nashindwa hata kuelezea, siamini kiasi hiki nilichoshinda ila ndiyo imetokea, inabidi niamini tu,” alisema.

Mshindi huyo ambaye alikuwa akizungumza na Mr Sokabet, aliongeza kuwa kiasi hicho cha fedha atakitumia katika shughuli zake mbalimbali na ataendelea kushiriki katika mchezo huo wa kubahatisha kwa kuwa fedha alizopata zimemsaidia sana.
“Yaani nilivyoshinda kuna watu wangu wa karibu walikuwa hawaamini juu ya michezo hiyo, wapo waliotamani wangeshinda wao, imebidi nianze kuwafundisha wengine kushiriki, mimi sina kinyongo nimeanza kuwapa maelekezo jinsi ya kushiriki.
“Unajua mimi bado sina familia, hivyo nimekuwa nikitumia muda wangu wa ziada baada ya kazi kutembelea tovuti ya Sokabet na kuwafuatilia katika mitandao mbalimbali, huko ndipo nilipojifunza, niwashauri tu washiriki wengine kuwa wasikate tamaa kwani wanaweza kupata ushindi, niwaambie tu Sokabet ni kampuni ya ukweli kwani bada ya kushinda wala sikupata longolongo nyingine zozote za za kupata fedha zangu,” alisema.
Akizungumzia kuhusu ushindi huo, Mratibu Masoko wa Sokabet, Franco Ruhinda alisema huo ni mwendelezo wa wao kuwapa faida Watanzania na washiriki wengine wote wanaobashiri.
Franco alisema ili kubashiriki washiriki wanaweza kutembelea na kujiandikisha kupitia tovuti ya www.sokabet.co.tz au kwa njia ya simu ya mkononi kwa kupiga *148*89#
“Kupitia SMS pia unaweza kushiriki kwa kutumia namba 15800, unachotakiwa kufanya ni kutuma neno SOKABET kwenda namba 15800. Kuwakumbusha tu namba ya kampuni ya Sokabet ni 335757,” alisema Franco.
Na Mwandishi Wetu