KUTOKANA na kile alichosema amechoshwa kuibiwa wanaume wake anaokuwa nao kwenye uhusiano, staa wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ameamua kubadili gia angani ambapo kwa sasa yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume wa kawaida ambaye siyo staa na hawezi kumwanika hadharani.
Akichezesha taya na Star Mix, Nisha alisema amekuwa akichukuliwa wanaume wake na wasanii wenzake kwa kuwa tu wanawafahamu hivyo kwa sasa ili kukomesha tabia hiyo ya kuibiwa ameamua kuwa na mtu ambaye siyo maarufu kabisa na penzi lao litakuwa la siri.
“Niko kwenye uhusiano na mwanaume wa kawaida kabisa maana nimechoka kuibiwa, siko tayari kumweka hadharani maana ndiyo mwanzo wa kukwapuliwa,” alisema Nisha.
NA GLADNESS MALLYA