Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group na mhamasishaji maarusu Afrika Mahsriki na Kati, Eric Shigongo amefanya mkutano na wanafunzi wa Chuo Cha Afya Muhimbili jijini Dar es Salaam na kutoa elimu ya ujasiriamali kwao na namna ya kutimiza ndoto zao, huku akijitolea mfano yeye mwenyewe kuwa kilichomfanya afanikiwe ni kipaji tu na si vinginevyo.
Aidha pia Shigongo amewaasa wanafunzi hao kujijengea dhana ya kusoma vitabu mara kwa mara na kama wanaona uvivu basi watumie hata mtandao wa kijamii wa Youtube, ili waweze kujifunza mambo mpya kila kukicha.