×

Lowassa, Mbowe, Sumaye Wamuombea Kura Mwalimu

VIONGOZI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ngazi ya Taifa wakiongozwa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe wamemuombea ridhaa ya kupigiwa kura na wananchi, Katibu Mkuu wa chama hicho kwa upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu anayewania ubunge wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Prof Jay: 

“Uwezo na sera za Mtulia tunazijua, nawza kutumia maneno makali lakini huo ndiyo ukweli, amewadharau sana watu wa Kinondoni. Tanazania nzima itatushangaa na tutakuwa tumeidharirisha Demokrasia, bora kuzungumza mengine kuliko habari za Mtulia.”

 

Ester Matiku.

“Inawezekana kabisa 2015 tulimchagua Mtulia kimakosa, Bwana amempta pepo la kujiuzulu, tumeletewa Salum Mwalimu. Februari 17, 2018 itakuwa ndiyo mwisho wa kuchagua watumishi wasaliti, tukampigie kura Mwalimu.”

Godbless Lema;

“Tunapokuja kumuombea Salum Mwalim ubunge hatuji kumtafutia ajira, tunakuja kutengeneza alama ya Demokrasia kwa siku zijazo, kuna wakati watakuwa walinda kura wazuri siku za usoni.”

 

Sumaye;

“Kama wewe ni mbunge halafu umehama chama, basi haufai. Hizo pesa za kurudia uchaguzi zingeweza kuleta miundombinu ikwa wananchi. Katiba inaruhusu kutoa maoni lekini leo ukitoa maoni yako unaambiwa mchohcezi. Vikao vya bunge hatuvioni kwenye Televisheni. Je, hii katiba ilibadilishwa ili kuzuia bunge lisionyeshwe?”

 

 

NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

 

Makonda Amwaga Machozi Mbele Ya Familia Iliyotapeliwa