

Emanuel Okwi amefunga goli lake la 12 katika Uwanja wa Taifa katika mechi za Ligi Kuu Tanzania bara leo wakati Simba ikishinda 4-0 dhidi ya Majimaji.

Okwi ameendeleza utawala jijini Dar es Salaam kwa kufunga magoli yake 12 katika viwanja viwili. Raia huyo wa Uganda hajafunga goli hata moja nje ya mkoa wa Dar katika mechi za ligi.
Kwa sasa anashikilia rekodi ya mchezaji pekee mwenye magoli mengi aliyofunga kwenye uwanja mmoja, amefunga magoli nane (8) kwenye uwanja wa Uhuru na mengine manne akifunga kwenye uwanja wa Taifa.

Amefunga mechi nne mfululizo ambazo Simba imecheza kwenye uwanja wa Uhuru, hajafunga katika mechi mbili ambazo amecheza nje ya uwanja wa Uhuru (Mbao 2-2 Simba, Stand United 1-2 Simba).
