×

GLOBAL HABARI: RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MAZISHI YA JAJI KISANGA


Rais John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli, wameongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa Jaji mstaafu Robert Kisanga aliyefariki Dunia January 23 mwaka huu.

 

Rais Magufuli amefika nyumbani kwa Marehemu Jaji kisanga na kupokelewa na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Juma na kisha kuweka saini katika kitambu cha maombolezo kabla ya kumfariji mjane wa marehemu Mama Maria Kisanga.

 

Baada ya hapo Rais Magufuli na Mkwewe wamefanya sala maalumu ya pamoja na familia ya marehemu Kisanga kwa ajili ya kumuombea marehemu huyo. Jaji kisanga ambaye aliwahi kuwa jaji wa Mahakama ya rufaa alifariki Dunia January 23 mwaka huu katika hospitali ya Regency alipokuwa akipatiwa matibabu.

 

Katika hatua nyingine Rais Magufuli leo amesali dominika ya Jumapili katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay akiwa na mke wake Mama Janeth Magufuli na mke wa waziri mkuu Marry Majaliwa. Subscribe muda huu www.youtube.com/user/uwazi1 Install #GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe http://www.youtube.com/c/uwazi