×

Chadema Wapigwa Barua Uchaguzi Kinondoni – Video

Wakati kampeni za uchaguzi jimbo la Kinondoni zikiendelea, Chadema wamepewa barua mbili za malalamiko na msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli, kikidaiwa kuvunja kanuni za maadili ya uchaguzi.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila amesema wamepokea barua hiyo jana, yenye malalamiko yaliyotolewa na Chama cha Wananchi (CUF).

 

Madai mengine ni kwamba viongozi wa CUF wanakuja katika mikutano yetu na kukaa meza kuu na kupanda katika majukwaa. Pia CUF wanadai Chadema inawatumia viongozi wao kupita nyumba kwa nyumba kuiombea kura Chadema wakiwa na sare za CUF.