RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameeleza kusikitishwa kwake na wafungwa ambao aliwasamehe hivi karibuni kwa vitendo vya baadhi yao kurudia kufanya makosa ya uhalifu na kupelekwa tena magerezani.
Rasi ameyasema hayo leo wakati akihutunia kwenye sherehe ya kilele cha wiki ya sheria jijini Dar es Salaam.
“Wafungwa wamekuwa wakiigharimu serikali pesa nyingi kwa ajili ya kuwahudumia, kiasi ambacho ni kikubwa cha kingeweza kusaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Sasa inabidi mahakama ziangalie adhabu mbadala kwa wafungwa mathalani wenye makosa madogo madogo.
“Nimesikitishwa kusikia baadhi ya wafungwa niliowapa msamaha wamerudi kwenye uhalifu, hii inaonesha kuwa wakiwa gerezani hawapati mafunzo stahiki , hii ni changamoto kwa wenzetu wa magereza, inabidi mfumo ubadilike, lengo la kufunga ni kuwafunza.
“Hii inaaonyesha kuwa wafungwa wakiwa jela hawapati mafunzo ya kutosha, wangekuwa wanalimishwa vizuri wanafanya adhabu za kutosha, wasingekuwa wanarudishwa huko, wanatakiwa wapewe mafunzo kweli kweli ili wasirudie makosa,” alisema Rais Magufuli.