Mshambuliaji wa timu ya Kibamba Worious Emmanyel, Athanas (kulia) akimtoka beki wa Mpakani FC, Haruna Ramadhani, timu hizo zilipopambana katika mechi ya fungua dimba ya Tulia Cup, katika Uwanja wa Kibwegele, Kibamba Dar es Salaam, juzi.
Katibu wa Kamati ya Uratibu wa Michuano ya Tulia Cup, Moreen Ngasala akimkaribuisha Diwani wa Kata ya Kibamba (CHADEMA), Ernest Mgawe (kulia) baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Mpiga wa Kibwegele, katika ufunguzi wa michuano hiyo.
Kibamba Warious na Mpakani FC wakiwa tayari kwa mtanange.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Elizabeth Majige aakisalimiana Katibi wa Siasa na Uenezi Kata ya Kibamba Clement Mgabo walipokutana kwenye uzinduzi wa michuano hiyo.
Mgeni rasmi akienda kukagua timu ili mpambano uanze.Mgeni rasmi akisalimia wachezaji wa timu ya Kibamba Warious.
Mgeni rasmi akiwa na baadhi ya viongzi baada ya kukagua timu.
Mgeni rasmi akizungumza kufungua michuano hiyo ambayo leo kuu ni kuwaweka vijana pamoja na pia kuchangisha vifaa na fedha kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Mtaa wa Hondogo katika Kata hiyo ya Kibamba. Mgeni huyo rasmi aliahidi kuchangia mifuko mia moja ya saruji.
“Vipi umenusurika?’ Mwamuzi akimuuliza mchezaji huku akimpapasa baada ya mchezaji wa timu ya Kibamba Warious baada ya kuchezewa vibaya na mchezaji wa Mpakani FC.
Kipa wa Mpakani FC akiuangalia mpira wakati ukiingia kimiani kufuatia penati iliyopigwa na mchezaji wa Kibamba Warious kutokana na mchezaji wa timu hiyo kufanyiwa rafu katika eneo la hatari.