×

Wanafunzi NIT Wapoteza Fahamu Baada ya Kuona Jeneza la Akwilina- Video

Mmoja wa wanafunzi hao akiwa amepoteza fahamu baada ya kuona jeneza lenye mwili wa Akwilina.

MAJONZI, VILIO na simanzi vimetawala wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini aliyeuawa kwa kupigwa risasi Feb 16, 2018.

Wanafunzi wakizidi kuzirai.

Baada ya mwili wa marehemu kuwasili katika viwanja vya NIT kwa ajili ya kuagwa, wanafunziwa chuo hicho walianza kulia kwa majonzi na uchungu huku wengi wao wakioanguka na kupoteza fahamu kutokana na kuguswa na msiba huo uliotikisa taifa zima la Tanzania.

Waombolezaji wakilia kwa uchungu.

Mwili wa Akwilina umeagwa leo katika viwanja vya Chuo cha NIT na kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Rombo Mashati kwa mazishi.

…Wakizidi kuanguka.
Akwilina alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema.
Hakika ni majonzi na simanzi.

 

Global Publishers na Global TV Online inatoa pole kwa ndugu, marafiki, wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba wa Akwilina.

 

Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi roho yua marehemu. AMEN!

 

Dada wa marehemu akwilina akisaidiwa.

PICHA NA RICHARD BUKOS | GPL

TAZAMA VIDEO YA TUKIO ZIMA LA KUAGA MWILI WA AKWILINA