×

Beki Mbao: Kichuya, Okwi Walituvuruga

Kikosi cha timu ya Mbao.

BEKI wa Mbao FC, David Mwasa amefunguka kuwa mabao mawili ya haraka ambayo yalifungwa na Simba kwa kipindi kifupi ndiyo yaliyowatoa mchezoni.

 

Simba ilitumia dakika nne kufunga mabao mawili ndani ya kipindi cha kwanza ambapo bao la kwanza lilifungwa na Shiza Kichuya (37) na Emmanuel Okwi (41). Mwisho wa mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Akizungumza na Championi Jumatano, beki huyo alisema awali walianza vyema lakini kitendo cha Simba kufunga tu ndiyo kiliwatoa mchezoni kabisa. Beki huyo alisema kwa sasa anaangalia majukumu yaliopo mbele yao kuhakikisha timu yao inakuwa na nafasi ya kufanya vyema.

 

“Unajua Simba siyo wa kutisha sana ila mbinu tu walituzidi kama kufunga yale mabao mawili ya haraka, wakatuchanganya, kwa sasa tunaangalia majukumu yaliyopo mbele yetu tuweze kufanya vizuri,” alisema Mwasa.