
MSHAMBULIAJI wa Simba, John Bocco amefungukia tuzo yake ya uchezaji bora aliyokabidhiwa juzi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar, kwa kusema kuwa imempa chachu ya kujituma zaidi.
Bocco baada ya kutangazwa kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora Mwezi Januari, juzi Jumatatu kabla ya mchezo wa timu yake dhidi ya Mbao, alikabidhiwa King’amuzi cha Azam TV na pesa shilingi milioni moja.
Akizungumza na Championi Jumatano, Bocco amesema kuwa, tuzo hiyo imempa changamoto zaidi ya kujituma katika kuitumika timu yake, huku akiwashukuru wachezaji wenzake kwa ushirikiano wanaompa. “Nashukuru Mungu kwa tuzo hii ambayo nimeipata nadhani ni chachu kwangu kuweza bidii na kujituma zaidi katika kuitumikia timu yangu iweze kufanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu.
“Pia nawashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano wanaonipa ambao unanisaidia kuweza kufanya vyema katika kila mechi tukiwa na lengo la kuisaidia timu yetu, nawaomba tuendelee kupeana ushirikiano ambao utatusaidia kuivusha timu yetu,” alisema Bocco.
Stori na Khadija Mngwai