×

Maujuzi ya Kessy Noma, Awapa Mzuka Yanga SC

Kikosi cha timu ya Yanga. Beki wa pembeni wa timu hiyo, Hassan Kessy wa kwanza aliechuchumaa.

AKICHEZA kwa kiwango kikubwa huku akiifungia na kuitengenezea mabao Yanga, beki wa pembeni wa timu hiyo, Hassan Kessy ametamka kuwa bado kiwango chake anachotaka kuonyesha hakijafikia huku akidai ubingwa wa msimu huu wa Ligi Kuu Bara utatua Jangwani.

 

Kauli hiyo, aliitoa mara baada ya mechi ya ligi dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani humo, Yanga ilishinda mabao 2-1 huku Kessy akifunga bao la pili.

 

Beki huyo, hivi karibuni alianza kupewa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza na kumuweka benchi, Juma Abdul aliyerejea kikosini baada ya kupona majeraha.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kessy alisema anafurahia sapoti kubwa anayoipata hivi sasa kutoka kwa mashabiki wa Yanga ambayo imemfanya yeye aendelee kucheza kwa bidii katika kuipa mafanikio timu hiyo.

 

“Mwanzoni nilikutana na upinzani mkubwa lakini bila ya kujali na kukata tamaa nilivumilia nikiamini ipo siku nitaaminika na kupata nafasi ya kucheza.

 

“Nashukuru hivi sasa nimeaminika na kocha na kunipanga katika kikosi cha kwanza, hivyo basi sitaki nirudi huko, ni lazima niipambanie timu yangu kwa kufunga na kutengeneza nafasi za kufunga mabao na kama unavyoona nimeanza vizuri nafunga na kutengeneza nafasi.

 

“Niwaambie Wanayanga kuwa, wala wasiogope bado ubingwa wetu wa ligi upo na hilo linawezekana kabisa kutokana na umoja na ushirikiano uliopo katika timu yetu, kikubwa waendelee kutusapoti,” alisema Kessy.

 

Kessy hadi hivi sasa amefunga bao moja katika ligi huku akitengeneza nafasi na lingine la Kombe la FA na Kombe la Mapinduzi huku akitengeneza nafasi zaidi ya saba za mabao.