×

Wafanyabiashara wa Korea, Tanzania Wamtembelea Balozi Matilda

Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Matilda Masuka (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya wafanyabiashara hao.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika ofisi ya balozi huyo.
Balozi Matilda (kushoto) akimkabidhi mfanyabiashara wa Korea mfuko wenye Mlima Kilimanjaro ulioko Tanzania.
Diwani na mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri ya Wilaya  ya Sengerema, Mathew Lubongeja (kushoto) akimwonyesha Balozi Matilda picha za mkutano wa wafanyabiashara hao.

TIMU ya wafanyabiashara wa Korea na Tanzania waliopitisha mkataba wa kushirikiana, wakiongozwa na mratibu wa timu hiyo, diwani na mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri ya Wilaya  ya Sengerema, Mathew Lubongeja, ambaye kwa sasa yuko nchini Korea, walimtembelea  Balozi wa Tanzania nchini humo, Matilda John Masuka.

 

 

Wafanyabiashara hao ni wa kampuni  mbili za Tanzania ambazo ni  Blue Mark iliyo chini ya Mkurugenzi wake, Eric Shigongo,  na JONTA Investment  Ltd  iliyo chini ya Mkurugenzi  John Elias Ntalimbo wa Shinyanga. Kampuni hizo zimesaini mkataba wa kuungana na kufanya kazi na kampuni ya Sungwoo I. D. Construction Co. Ltd ya  Korea ya Kusini inayoongozwa na Jeun Ki  Wook ambapo  mkataba huo unahusu ushirikiano katika kukuza sekta ya ujenzi.

 

 

Kabla ya kumtembelea balozi huyo,  wafanyabiashara hao  walikuwa na mkutano uliofikia makubaliano ya ushirikiano wa kimaendeleo baina ya mji wa Sengerema, mkoani Mwanza, na Jiji la Gyeongsan la Korea Kusini.