
MJI mdogo wa Polokwane upo Kaskazini mwa jimbo maarufu zaidi nchini Afrika Kusini la Gauteng.
Makao makuu ya Gauteng ni upande wa jiji kubwa zaidi Afrika Kusini la Johannesburg. Kutoka katika jiji hilo ni mwendo sahihi wa saa tatu kufika katika mji huo mdogo.
K w a w a n a o f u a t i l i a michezo, P o l o k w a n e ni kati ya miji iliyokuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika kwa mara ya kwanza na mwisho hadi sasa barani Afrika, hiyo m w a k a 2010.
Maana ya neno Polokwane ni “eneo s a l a m a ” , huko ndiyo anaishi Mtanzania, Abdi Banda, kijana aliyechipukia kisoka katika klabu ya Coastal Union ya Tanga.
Banda anaishi Afrika Kusini katika mji huo wa Polokwane ingawa maisha yake yamekuwa ni kutembea kutoka mji mmoja kwenda mwingine na si rahisi kubaki Polokwane angalau kwa wiki mbili mfululizo kutokana na majukumu yake.

Polokwane timu maarufu zaidi ni Polokwane City ambayo hata hivyo kipindi hiki imekuwa ikipoteza umaarufu kutokana na mwendo mzuri ilionao Baroka FC katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini pamoja na michuano mingine ya makombe mbalimbali.
Mwendo mzuri wa Baroka FC unaifanya timu hiyo kuzidi kujizolea mashabiki na kupata sapoti kubwa kutoka kwa watu wa eneo la Polokwane. Banda ni beki wa timu ya Baroka FC, ni beki tegemeo na sasa kivutio cha mashabiki wengi wanaomuona ni kama mchezaji staa na tegemeo namba moja katika kikosi hicho.
Umaarufu wa Banda umekuwa ukikua kwa kasi kubwa na hii inatokana na kuaminika zaidi na benchi la ufundi na namna ambavyo amekuwa akiifanya kazi yake kwa ufasaha mkubwa.
Championi kama ilivyo kawaida yake, limeamua kufunga safari hadi nchini Afrika Kusini kumshuhudia Banda akiwa kazini na kujifunza mengi kuhusiana na kazi yake anayoifanya.

Wakati a k iondoka Tanzania na kujiunga na Baroka FC, ilionekana ni vigumu Banda kufika mbali, lakini sasa ni gumzo kuu na tegemeo katika kikosi hicho na tayari ameanza kuwa kivutio kwa baadhi ya timu kubwa za Afrika Kusini.
Katika mahojiano hayo ya moja kwa moja hapa Afrika Kusini, Banda anazungumza mengi ambayo asilimia 99 hukuwahi kuyasikia.
Anaeleza safari yake ya Afrika Kusini, hatua alizopiga na chamgamoto. Tutakwenda taratibu kwa hatua k u
jua mengi yakiwemo yale ambayo aliyapata kama changamoto wakati akiwa anacheza Tanzania na nini sasa anataka baada ya hatua nzuri aliyopiga na Baroka FC.
Banda anasema, kitu cha kwanza ambacho kilimsaidia kupiga hatua na kufika mbali ni malengo makubwa aliyokuwa amejiweka kutaka kutoka nje ya Tanzania na kucheza nje.
CHAMPIONI: Malengo wengi wanaweka lakini wameshindwa kuyatimiza, wewe ilikuwaje ukafanikiwa?
BANDA: Kila mmoja huwa anapanga kivyake lakini utekelezaji wa malengo ndiyo tatizo kubwa zaidi. Mimi nataka kufuyafikia malengo yangu.
CHAMPIONI: Wakati ukiondoka kuja Afrika Kusini haukupewa nafasi ya kufanya vizuri, unafikiri Tanzania ulikosea wapi?
BANDA: Tanzania kuna mambo mengi sana ambayo yanamfanya mchezaji ashindwe kucheza. Naamini tutayazungumzia lakini vitu ni tofauti sana.
CHAMPIONI: Wewe ulisifika kwa utukutu na mara nyingi ulionekana hausikilizi?
BANDA: Hapa Afrika Kusini ukiwaambia mimi ni mtukutu watashangaa sana, lakini ukweli mimi ni mpambanaji na mtu ninayetaka kushinda kwa kila ninachokifanya au kukutana.
CHAMPIONI: Umeweza vipi kuendana na utamaduni wa soka la Afrika Kusini kwa maana ya nidhamu ya juu, mambo kwa mpangilio wakati ulizoea Tanzania mambo ya kubabia?
BANDA: Kweli mambo ni kwa mipangilio, ratiba na utaratibu sahihi. Nimeona huu ni utamaduni na utaratibu sahihi ambao wanatumia, ni lazima niufuate na naona ni vizuri.
CHAMPIONI: Tanzania hukufuata utaratibu, hapa uliweza vipi, ilikuwa ina shida kwako au ulichukua muda gani kuendana na wenzako?
BANDA: Kulikuwa na ugumu, lakini kwangu ilikuwa kidogo sana kwa kwa kweli. Baada ya muda nikaweza kuendana nao. Napenda kufuata utaratibu tokea nikiwa Tanzania. Lakini kama viongozi wako hawafuati utaratibu, wachezaji wenzako hali kadhalika, unafikiri wewe utafuataje utaratibu kwa asilimia mia? Hapa watu wanafuata utaratibu na mimi naendana nao.
CHAMPIONI: Udhibiti wa suala la nidhamu ukoje hapa?
BANDA: Nidhamu ni jambo namba moja katika mpira wa Afrika Kusini. Hawa jamaa wako tayari kukuondoa katika kikosi mara moja bila ya kuangalia sura kama utafanya utovu wa nidhamu, yaani hata kama wanakutegemea kwa asilimia elfu moja.
STORI NA SALEH ALLY | GLOBAL PUBLISHERS