






BODI ya barabara ya Mkoa wa Dar es Salaam, inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda ambaye ni Mwenyekiti wa bodi hiyo imeanza mkutano wake kujadili masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuboresha miundombinu katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Anatouglo, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Makonda amempongeza mkandarasi aliyejenga barabara za kuingia na kutoka katika Kituo cha Mabasi cha Makumbusho, na kueleza kwamba wakandarasi wengine wanapaswa kuiga mfano huo.
Mbali na mambo mengine, mkutano huo pia umelenga kujadili matumizi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya maboresho ya barabara zinazopita katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari.
Wajumbe waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na madiwani, wabunge, wakuu wa wilaya na wadau wengine wa maendeleo wa mkoa huo.
NA DENIS MTIMA/GPL