×

KOCHA AL MASRY AMUOGOPA OKWI

KOCHA Mkuu wa Al Masry, Hos­sam Hassan akiri kuifahamu Simba vizuri kwa kuwa ametumia muda mwingi kuangalia video za mechi zao lakini hofu yake imekuwa kwa Em­manuel Okwi.

 

Hossam ambaye ni mchezaji wa zamani wa Misri na Zamalek alikutana Simba mwaka 2003, ka­tika Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa mchezaji na timu yake kuon­doshwa kwa penalti na Simba kutinga makundi ya michua­no hiyo mikubwa Afrika.

 

Hossam alisema; “Wapinzani wetu tunawaelewa vizuri kwa sababu tume­tumia muda mwingi kuangalia video za mechi zao lakini wametutisha kidogo kwenye usham­buliaji kwa kuwa wanaonekana wao ni bora sana.”

 

“Pale wana wache­zaji wazuri sana, lakini tutajitahidi kukabiliana nao wa­situletee madhara,” alisema Hossam.

Na Ibrahim Mussa, Dar es Salaam