×

Yanga yaanika kikwazo kabla ya kuwavaa Waswana

BENCHI la ufundi la Yanga chini ya kocha wake mkuu, George Lwandamina raia wa Zam­bia limeeleza kutofurahia ratiba ya kikosi chake kinachokabiliwa na mch­ezo mgumu wa marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ugenini nchini Botswana.

Yanga leo Jumatatu itashuka uwanjani kucheza na Stand United ya Shinyanga ikiwa ni siku mbili tu Ijumaa iliyo­pita kucheza na Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi huku Yanga wakishinda kwa mabao 3-0.

Kikosi hicho pia Jumamosi hii kitakuwa na kibarua cha kucheza ugenini dhidi ya Township Rollers ya Bot­swana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Yanga kwenye mchezo wa kwanza walipoteza kwa mabao 2-1.

Akizungumza na Championi Ju­matatu, Mzambia huyo amesema anahofia kutopata muda wa ku­tosha kuwaandaa wachezaji wake kwa ajili ya mchezo huo ambao ni lazima Yanga iibuke na ushindi wa mabao matatu ugenini ili iweze kufuzu hatua ya makundi.

 

Said All, Dar es Salaam