



ENEO la Kariakoo kama ilivyozoeleka ni eneo ambalo shamrashamra zake ni nyingi, ikiwa ni pamoja na watu, magari na shughuli nyingine mbalimbali za kijamii. Ni eneo lenye shughuli nyingi zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ya Jiji la Dar es Salaam.
Kamera yetu leo ilipita eneo hilo na kunasa taswira mbalimbali za shughuli zifanyikazo eneo hilo hasa kwa upande wa magari ya mwendo kasi.
Zifuatazo ni picha zinazoonyesha taswira ya eneo hilo na magari ya mwendokasi yakipita katika barabara zake maalum.
Na Denis Mtima/Gpl