KUFUATIA sakata la maji yanayodaiwa kuwa na sumu yanayotirirshwa na kiwanda cha Murzah kilichopo maeneo ya Vingunguti jijini Dar es Salaam, Global TV Online imefunga safari mpaka katika eneo linalotiririka maji hayo maeneo ya Tazara na kuzungumza na wananchi, Mwenyekiti wa Serikali za mitaa, Msemaji wa kiwanda hicho pamoja na mama ambaye mwanae aliathirika kwa kubabuka miguu kutokana na maji hayo.
Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Faru, Simba Said Simba, amethibitisha na kusema watu ambao wamewahi kupata madhara makubwa kutokana na maji hayo, huku akibainisha kuwa chanzo cha maji hayo ni kifusi kilichoziba njia ya maji ambacho kilitokana na kuvunjwa kwa Magodauni.
Mama wa mtoto aliyebabuka kutokana na maji hayo amesema kuwa siku ya tukio mwanae alikuwa akienda shule na baada ya kuvuka maji hayo, ambapo baada ya kuvuka ngozi ilianza kutoka na kubabuka na mpaka sasa bado hajapona. Msemaji wa kiwanda hicho, amesema malalamiko ya wakazi hao hayahusiani na kiwanda chao.