×

PIGO SIMBA: MKUDE AUMIA VIBAYA MAZOEZINI – VIDEO

KIUNGO mahiri wa Simba SC, Jonas Gerald Mkude leo alilazimika kubebwa baada ya kuumia kifundo cha mguu wake wa kulia katika mazoezi ya timu hiyo Uwanja wa Boko Veterani mjini Dar es Salaam.

 

Mkude aligongana na kiungo mwenzake, Muzamil Yassin wakati wa kugombea mpira na kuanguka chini huku akiugulia maumivu, kabla ya Daktari wa timu, Yassin Gembe kuingia uwanjani kumpatia huduma ya kwanza.

 

Lakini huduma hiyo haikumsaidia Mkude, kwani hakuweza hata kuukanyagia mguu ulioumia kiasi cha kubebwa kupelekwa kwenye chumba cha kuvalia nguo, kabla ya kurudishwa nyumbani kwa gari.

 

Dk. Gembe aliiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba atalazimika kusubiri hadi kesho ili kumfanyia vipimo Mkude ili kujua uzito wa maumivu yake.

PIGO SIMBA: MKUDE Alivyotoka Machozi Mazoezini Baada ya Kuumizwa