×

WATU 6 WA FAMILIA MOJA WALIOKUFA MKURANGA WAZIKWA DAR – VIDEO

WATU sita ambao ni ndugu wa familia moja wakiwa miongoni mwa watu 26 waliofariki kwa ajali ya gari usiku wa kuamkia jana Jumapili, Machi 25, 2018 katika Kijiji cha Mparange Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, wamezikwa leo Machi 26 katika Makaburi ya Machinjioni, Mtaa wa Mnyamani Vingunguti jijini Dar es Salaam ambapo Global Publishers ilikuwepo kwenye mazishi hayo.

Ajali hiyo ilisababisha pia watu tisa kujeruhiwa baada ya gari dogo (Hiace) lililokuwa  likitoka Mkuranga kuelekea Kimanzichana mkoani Pwani, kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba chumvi likitokea Mtwara kuelekea Dar es Salaam.

 

Watu hao waliofariki dunia na kuzikwa jijini Dar es Salaam ni, Mwajuma Aly, Abdallah  Athuman, Said Athuman, Nuru Yusuph, Halima Jabir na Yusra Said.

NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

VILIO Vyatawala Familia ya Watu Sita Waliokufa Ajali ya Watu 26