×

HATIMAYE DIAMOND AMALIZANA NA MWAKYEMBE, SHONZA – VIDEO

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz akiongea baada ya kukutana amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe na Naibu wake Juliana Shonza.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz Machi 27, 2018 amekutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe na Naibu wake Juliana Shonza na mazungumzo yaliyodumu kwa saa matatu katika ofisi za BASATA zilizopo jijini Dar es salaam.

Naibu  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Juliana Shonza akiongea na wanahabari.

Diamond Platnumz aliongozana na Mameneja wake watatu, Sallam Sharaf, Babu Tale na Said Fella ambapo wamezungumza kuhusu nyimbo za Diamond kufungiwa na kuelezana ukweli kuhusu mmomonyoko wa maadili kwenye nyimbo za muziki wa Bongo Fleva ambapo, Diamond amemhakikishia Waziri Mwakyembe kuwa atalinda maadili kwa nguvu zake zote hususani kwenye kazi zake.

Kwa upande mwingine Waziri Mwakyembe amezitaka taasisi zilizo chini ya Wizara yake kama BASATA, Bodi ya Filamu na TCRA kuitisha vikao mara kwa mara na wasanii ili kujadili masuala ya sanaa.

Hayo yanajiri katika kipindi ambacho Diamond Platnumz na Naibu Waziri wa Habari, Mhe. Juliana Shonza kupishana kauli, na kwa kikao hicho cha masaa matatu kimemaliza tofauti zao.

Soma zaidi taarifa hiyo;

Diamond amalizana na Serikali.

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on