
Mdau wa mitindo ya mavazi na urembo, Salma Kader maarufu kama Salma Collection jana aliwatembelea watoto yatima wa Kituo cha Abubakar Islamic Foundation kilichopo Mingoi Bagamoyo na Sifa Foundation kilichopo Vikawe Bagamoyo mkoani Pwani na kubadilishana nao mawazo.

Salma ambaye alikuwa ameambatana na watoto wake watatu katika ziara hiyo baada ya kubadishana mawazo na watoto hao na kujionea changamoto zinazowakabili aliwakabidhi msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo sabuni, mafuta ya kupakaa na kupikia, unga, sukari, maharage, viungo, mchele, ndizi, chokleti.

Watoto hao baada ya kubadilishana mawazo na kupewa moyo wa kuwa na mafanikio makubwa katika maisha yao walionesha furaha na kumkaribisha tena siku nyingine wakati akiwaaga.

Nao walezi wa vituo hivyo walimshukuru Salma kwa kuwakumbuka watoto hao haswa kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.