MUUZA nyago mwenye umbo matata Bongo, Sasha Kassim amewaonya wasanii ambao wamekuwa wakitelekeza familia zao sababu ya umaarufu walionao na kuwaona wazazi wao hawana thamani.
Akipiga stori na paparazi wetu akiwa kwao Mwanza, Sasha alisema ameamua kujichimbia huko kwa muda kwa lengo la kuijulia hali familia yake na amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara, ila amehuzunishwa na wasanii ambao wanazitelekeza familia zao sababu tu ya kupata jina.
“Nimekuwa nikisikia wasanii wengi acha kwa leo nisiwataje. Wana makubwa lakini hawana mpango na familia zao kwa salamu wala kuwasaidia kiuchumi hii si sawa, haya maisha ya ustaa yana kupanda na kushuka hakuna aijuaye kesho, hivyo tusijisahau,” alisema Sasha.
Stori: Mayasa Mariwata