×

REKODI ZAONYESHA UGUMU WA MECHI MTIBWA VS SIMBA

KIKOSI cha Simba leo kinashuka uwanjani kupambana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na rekodi mbalimbali zinazoonyesha ugumu kila mara timu hizo zinapokutana kwenye uwanja huo.

Rekodi zinaonyesha kuwa tangu msimu wa 2013/14 mpaka sasa, Simba imeshinda mara moja tu katika uwanja huo lakini mechi nyingine zili­zobaki zimezaa sare.

 

Msimu wa 2013/14 timu hizo zilitoka sare kwa kufungana bao 1-1, 2014/15 matokeo pia yakuwa ni sare ya 1-1 lakini 2015/16 Simba ilifanikiwa kupata ushindi uwanjani hapo wa bao 1-0.

Hata hivyo, msimu uliopita wa 2016/17 Simba ilikumbana na kizingiti katika uwanja huo baada ya kushindwa kupata ushindi kwa mara nyingine tena ambapo matokeo yalikuwa ni 0-0.

 

Kutokana na rekodi hizo, lol­ote linaweza kutokea uwanjani hapo ukizingatia pia timu hizo zimetoka kupata ushindi katika mechi zao za ugenini zilizoche­za hivi karibuni.

Simba iliifunga Njombe Mji mabao 2-0 wakati Mtibwa Sugar iliifunga Singida United mabao 3-0, hivyo hali hiyo pia itasababisha mchezo huo kuwa mgumu.

 

SweetbertLukonge, Dar es Salaam