GERARD Piqué sasa ni beki anayekamata namba tatu (pacha) kwa kufunga mabao mengi zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Bao lake aliloifungia Barcelona dhidi ya Roma, lilikuwa la 12 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, na kumpeleka hadi namba tatu pacha katika orodha ya mabeki waliofunga mabao mengi zaidi katika historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Piqué aliiwezesha Barcelona kushinda mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa robo fainali dhidi ya Roma Jumatano iliyopita .
HAWA NDIYO MABEKI WAFUNGAJI BORA ZAIDI WA WAKATI WOTE UEFA:
Roberto Carlos 16
Iván Helguera 15
Dani Alves 12
Gerard Piqué 12
Christian Panucci 11
Sergio Ramos 11