×

Kiben Ten Amchumbia Blac Chyna Instagram

Blac Chyna akiwa na YBN Almight Jay

MPENZI mpya wa mwanadada anayekimbiza kwenye ulimwengu wa mitindo, Blac Chyna, 29, anayefahamika kwa jina la YBN Almight Jay, mwenye miaka 18 ‘Kiben Ten’, hivi karibuni ameonyesha nia ya kumuoa mwanadada huyo kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, baada ya kumuuliza swali Chyna kama atakubali amuoe au la.

 

YBN ambaye yupo katika uhusiano na Chyna kwa takribani mwezi mmoja baada ya Chyna kuachana na mzazi mwenziye Rob Kardashian, waliyezaa naye mtoto wa kike aitwaye Dream, aliandika hivi; “Will you marry me?”, huku akiambatanisha picha nzuri ya mrembo huyo.

 

Hata hivyo, Chyna hakujibu lolote lile katika posti hiyo zaidi ya ku-like, lakini wawili hao wamekuwa wakionekana maeneo mbalimbali wakila bata na wakiwa katika mahaba motomoto.

NEW YORK, Marekani