IKIWA leo Aprili 13, 2018 ni Kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Nyerere, Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwl. Nyerere kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam kimeandaa kongamano maalum la kumuenzi muasisi huyo wa Taifa hili.