Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, akizungumza kwa niaba ya serikali akiwapa pole ndugu, jamaa na marafiki wakati wa kuaga mwili wa msanii Agnes Gerald ‘Masongange’ katika viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar es Salaam leo.Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James, akizungumza wakati wa kuuaga mwili wa Masongange.Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba, akizungumza katika msiba huo.Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara, akizungumza katika msiba huo.Mwanamuziki Diamond Platnumz (kushoto) na msanii mwenzake Harmonize, wakizungumza wakiwa katika hafla hiyo ya kuuaga mwili wa Masogange.Ali Kiba akisalimiana na Kheri James.Diamond akisalimiana na Ali Kiba.Diamond alipowasili na timu yake ya Wasafi (WCB).Diamond akielekea kuuaga mwili wa marehemu.…Akitoka kuuaga mwili wa Masogange.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, leo ameongoza wananchi wa Dar es Salaam wakiwemo wasanii waliofika viwanja vya Leaders, Kinondoni, kwa ajili ya kuuaga mwili wa msanii Agnes Masogange ambapo miongoni mwao walikuwepo Ali Kiba, Diamond, Haji Manara, Kheri James.
Wengine ni Jacqueline Wolper, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Anti Ezekiel, na wengine.
Marehemu Masogange amesafirishwa leo kuelekea Mbeya ambako anatazamiwa kuzikwa kesho (Jumatatu).