
Majeruhi wa ajali ya basi la mwendokasi iliyotokea Februari 22, 2023, Osam Milanzi ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya afya yake kuimarika.
Taarifa ya kuruhusiwa kwa Osam, imetolewa Machi 28, 2023 na Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MOI), Patrick Mvungi.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Milanzi alipokelewa MOI Februari 22, 2023 ambapo alipata huduma za kibingwa katika kitengo cha dharura (EMD), ICU, HDU na wodi 2A.
“Ndugu Milanzi alipokelewa MOI akiwa ameumia maeneo ya kichwa, mguu wa kushoto, mkono na bega upande wa kulia.
“Ndugu Milanzi ataendelea na huduma kama mgonjwa wa nje na atarudi kliniki baada ya wiki mbili.
“Aidha, Tunatoa shukran za dhati kwa Watanzania wote, vyombo vya habari ambao kwa pamoja wameshirikiana nasi katika kumuombea na kumtangaza ndugu Osam Milanzi,” imeeleza taarifa hiyo.