×

Washindi Spoti Xtra Kukabidhiwa Zawadi Leo

WASHINDI wa shindano la Beats by Dre Orijino, linaloendeshwa na gazeti bora la michezo linalotoka kila Jumapili la Spoti Xtra, leo Jumatatu wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao walizojishindia kutokana na droo iliyochezeshwa Alhamisi iliyopita.

 

Washindi hao wanne ambao wanatoka mikoa tofauti ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam na Kibaha, walipatikana katika droo ambayo huwa inafanyika kila Alhamisi na kuonyeshwa moja kwa moja katika Kipindi cha Spoti Hausi ambacho hurushwa na Global TV Online.

 

Mhariri wa Gazeti la Spoti Xtra, Michael Momburi, amewataja washindi hao kuwa ni Fadhili Ramadhani mkazi wa Mkuranga aliyejishin­dia headphones orijino za Beats by Dre huku Juma Saleh wa Vingunguti, Godluck Mushi ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Ally Bobea kutoka Kibaha, wakijishindia jezi za timu wanazozipenda katika ligi kuu.

 

“Zawadi zinatolewa kwa wakati na kitu ambacho wasomaji wanatakiwa kukifanya ni kuhakikisha hawakosi nakala ya Gazeti la Spoti Xtra ambalo linatoka kila Jumapili kwa shilingi 500 tu na wata­pata maelekezo yaliyo ukurasa wa pili na kuweza kushiriki shindano hilo ambalo huwa linarushwa ‘live’ Global TV katika Kipindi cha Spoti Hausi kila siku ya Alhamisi,’’ alisema Momburi.

Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam.