×

Halima Burembo: Upinzani Mkishindwa Njooni CCM – Video

Mkutano wa Bunge la 11 umendelea leo mjini Dodoma ambapo wabunge walikuwa wakichangia bajeti ya Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano iliyopo chini ya Waziri, Profesa Makame Mbarawa na Naibu wake Atashasta Nditiye.

 

Mbunge wa Viti Maalum, Halima Bulembo amesema Rais Magufuli anafanya kazi nzuri na ametekeleza matakwa ya CCM na Ukawa hivyo wapinzani wakiona wameishiwa hoja wafunge milango na wajiunge na CCM na chama hicho kitawapokea ili kujenga nchi.