×

MASALA: Siyo Lazima Wabunge Wote ‘Tutoe Mapovu’ – VIDEO

Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala akichangia hoja kwenye bajeti ya Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano, amesema siyo lazima kila mbunge anaposimama kuchangia lazima azungumze kwa hasira ‘kutoa mapovu’, badala yake wanaweza kutumia lugha ya kawaida na Serikali ikayachukua mawazo yao na kuyafanyia kazi.

 

Masala ameitaka Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi iliyo chini ya Waziri, Profesa Makame Mbarawa na Naibu waziri wake, Atashasta Nditiye kutengeneza Barabara ya kutoka Nachingwea, kupitia Ruangwa Mjini kwenda Namichiga na kutokea Kiranjaranja yenye urefu wa Kilometa 100 ambayo ni muhimu kwa kuimarisha uchumi wa eneo hilo na maeneo ya karibu.

VIDEO: MSIKIE MASALA AKIFUNGUKA