×

Spika Tulia Amtwisha Mzigo Waziri Mkuu, Amtaka Atatue Mzozo wa Bodaboda na Bajaji

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Akson

 

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Akson amemtaka Mtendaji Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni ambaye Waziri Mkuu kulibeba sakata la katazo la madereva Bodaboda na Bajaji waliopigwa marufuku kuingia katikati ya jiji la Dar es Salaam.

 

Spika Tulia ametoa maelekezo hayo mara baada ya Mbunge wa Ukonga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jerry Silaa kulitaka Bunge kusimamisha shughuli zake na kujadili sakata hilo.

 

Mbunge huyo wa Ukonga alisema:

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa

“Mheshimiwa Spika, hata wewe juzi ulipokwenda Mbeya ulipokelewa na kundi kubwa la vijana wa bodaboda na maeneo mengine tunawategemea, Jijini Dar es Salaam kumekuwa na sintofahamu kuhusu kundi hili, naomba wenzangu waniunge mkono tulijadili,”

 

Akijibu hoja hiyo Spika Tulia amesema ili hoja ijadiliwe lazima iwepo ridhaa kutoka katika kiti chake na kuona kama inafaa na inabeba uzito wa kusitisha shughuli nyingine za Bunge na kujadiliwa, badala yake Spika Tulia alimtaka Waziri Mkuu kusimamia suala hilo.

 

“Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni ambaye ni Mheshimiwa Waziri Mkuu yupo hapa tunaomba ulibebe jambo hili na kutoa mwongozo ikiwemo magari ya Kigoma, ili watu wajue,” amesema Dk Tu

Leave a Comment