
MWILI wa mama mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Judith Mbibo Wambura ‘Lady Jaydee au Jide’, Bi. Martha Mbibo umefanyiwa ibada na kuagwa nyumbani kwake Kiwalani jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Bunda mkoani Mara kwa maziko.
Bi. Martha alifariki dunia juzi nyumbani kwake kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya saratani kwa muda mrefu.

Marehemu ameacha watoto wanane kati ya kumi ambapo wawili walishatangulia mbele za haki.

Katika familia hiyo, Jide ni mtoto wa tisa miongoni mwa hao kumi.


PICHA NA AMOS CRISPINE | GLOBAL TV ONLINE