MWILI wa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro umeagwa leo kwenye Msikiti wa Manyema uliopo Kariakoo baada ya kuswaliwa kisha kupelekwa nyumbani kwake Mbweni Luis utakapoagwa tena na baadaye kusafirishwa kwenda Kijijini Ihemi mkoani Iringa kwa mazishi yatakayofanyika kesho Jumapili.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisaini katika daftari la waombolezaji Mbweni jijini Dar es salaam, nyumbani kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Marehemu Abbas Kandoro aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati akitibiwa.
Gari lililobeba mwili wa marehemu.
Kandoro alieaga dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole mke Marehemu Abbas Kandoro, Mariam Kandoro nyumbani kwa marehemu Mbweni jijini Dar es Salaam leo Aprili 28, 2018.