
WATU watatu wamefariki dunia papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kugongwa na Basi la Kampuni ya Frester lenye namba za usajili T 720 DEV eneo la Katongo, Kata ya Rulanda wilayani Muleba mkoani Kagera leo Asubuhi Aprili 28, 2018 ambapo basi hilo lilikuwa likitokea Bukoba kuelekea Mwanza.
Vijana hao wamekumbwa na ajali hiyo wakati wakiwa njiani kwenda Madrasa huku miili yao ikiwa haijatambulika.

Kwa mujibu wa abiria waliokuwa kwenye basi hilo wamesema, chanzo cha ajali ni dereva wa basi alipokuwa akimkwepa mwendesha bodaboda hivyo kuwaparamia vijana hao akiwemo huyo bodaboda na kusababisha basi hilo kupinduka.

Abiria wote waliojeruhiwa kwenye basi hilo wameokolewa na wenzao huku zikifanyika jitihada za kuwapeleka Kituo cha Afya Kaigara na Hospitali ya rufaa wilayani Muleba.