MASHABIKI wa Simba wameendelea kutamba katika harakati za kutetea ubingwa na watani wao wa jadi Yanga katika mchezo wao leo katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Mashabiki hao wameonekana kujiamini kila shabiki akisema kuwa simba itachukua ubingwa na itawafunga watani wao katika mchezo wa jumapili. Simba na Yanga zitashuka dimbani katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.