
MKE wa Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete jana usiku alipata fursa ya kuhudhuria katika harusi ya staa wa Bongo Fleva, Alikiba na mkewe, Amina katika ukumbi wa Serena Hotel uliyopo Posta jijini Dar es Salaam ambapo aliungana na ndugu, jamaa na marafiki wa msanii huyo kusherehekea harusi hiyo.
Mama Salma alionekana kuchamka zaidi baada ya wimbo wa MAMA ulioimbwa na Alikiba na Christian Bella ulipoanza kupigwa ukumbini hapo. Mama Salma na wageni wengine walikuwa wakicheza huku yeye akicheza na mwanaye ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.
Katika sherehe hiyo pia inahusisha harusi ya mdogo wa Alikiba, Abdu Kiba na mkewe, Ruwayda ambao walifunga ndoa Jumapili iliyopita.