Rais Magufuli anaongea.
-Anaanza na Salaamu kwa wote waliohudhuria mabibi na mabwana.
– Nlitegemea kwakuwa kuna machifu hapa hii mvua ingekua imeacha kunyesha. Naona kweli imeacha kweli kuna amchifu walioiva.
-Nawashukuru TUCTA kwa kunialika kwenye sikukuu hizi. Natuminia fursa hii kuungana na waliotangulia kutoa pole kwa misiba ya viongozi vyama vya wafanyakazi na wafanyakazi waliotangulia
-Hii ni mara ya Kwanza kuja Iringa tangu nichaguliwe kuwa rais, nawashukuru kwa kunichagua. Wanairinga sina cha kuwalipa zaidi ya kusema tutashirikiana.
-1978 na 1979 nlijiunga na shule ya serikali ya Mkwawa, ukinambia kihesa makanyagio na kila sehemu napafahamu. najua namna ya kunywa ulanzi na komoni. Asanteni sana kwa kunitunza wana Iringa. Katika maisha yangu siwezi kuwasahau wanaIringa.
Leo ni siku ya wafanyakazi, napenda kutumia fursa hi kuwapongeza wafanyazi kwa mchango wenu mkubwa kwa mchango wenu wa kuletea nchi yetu maendeleo. Hingereni sana
-Serikali ya awamu ya tano itaendelea kushughulikia kero zenu na kuberesha masirahi yenu
-TUCTA imesema haitakuwa tayari kuwatetea wafanyakazi mabazazi yaani wazembe wafitini walevi mafisaidi nk. Nawashukuru. Nidhamu na uwajibikaji ni jambo mihumu.
– Mtumishi akiwa mvivu na mzembe anakuwa ni mnyonyaji.
-TUCTA wameomba kero za wafanyazi zishugulikiwe. Hoja zenu zote ni sahihi na serikali inazikubali na itazifanyia kazi.
-Leo nmeona bango la Walimu linasema wao wanaendelea kuhama bila kulipa pesa. Waziri mkuu anomba ulisimamie hilo. hatuwezi kuwa tunatoa maagizo halafu mtu mwingine aendelee kufanya hivyo. Tulishatoa maagizo mtu asihamishwe bila kulipwa. Naagiza tena viongozi ndani ya Serikali Wasihamishwe watu bila kulipa hela za uhamisho. NI matumaini yangu sitarudia tena kulizungumzia hili katika maisha yangu
-Serikali ya awamu ya tano imefanya mambo mengi;
1. Tumefanikiwa kudhibiti mfumko wa bei sasa ni 3.9. hii imekuwa njia nzuri ya kumsaidia mfanyakazi. Tutahakikisha bidhaa muhimu zinapatikana maeneo yote
2. Tunatoa elimu bila malipo kwa mwezi Bil23.8 kila mwezi miaka miwili tumetoa bil 714
3 tumelipa madenni ya mifuko ya jamii. mafai yalifika trilioni 1.6 n tumelipa trilioni 1.4
4. Tumelipa mazabuni
-Bil 900 madeni ya nje tunaendela kulipa na kwa miaka miliwi tumelipa zaidi ya trilioni 2
-Mishahara tunalipa Bil 564.501 baada ya kutoa wafanyakazi hewa, zamani tulikuwa tunalipa bil 777
-Tunatekeleza miradi mbalimbali ya Miundombinu kama SGR, Ujenzi wa meli ununuzi wa ndege, ujenzi wa Umeme, ujenzi wa mradi wa Stigler’s Gorge
-Mikopo, bandali mtwara, miradi ya maji, ukarabati wa reli, ujenzi wa rada. Kuna miradi mingi inaendelea.
– Tumebadili taswira ya utumishi wa umma. Watumishi hewa na wenye vyeti feki. Tumeweza kubaki na watumishi wenye sifa
-Tumeajiri watumishi wapya zaidi ya 18 elfu.
-Serikali itaendelea kuajiri na kutekeleza promotion za wafanyakazi.
– Ongezeko la ajira Milioni moja na laki nane na ishirini na sita elfu mia saba arobaini na tatu
-Viwanda 3,306 vimejengwa pwani kuna viwanda vipya 80
-Tumeshalipa malimbikizo kwa watu hamsini na mbili elfu mia nane hamsini na mbili yenye Bilioni themanini na sita na miatatu ishirini na tatu
-Yoyoyte mwenye madai halali atalipwa haki yake
-Ukijenga reli utabeba mizingo Mingi na kupata pesa. Ninaamini ukipeleka pesa hospital bil 266 afya zitaimarika.
-Mradi wa Stigler’s Gorge kwa trilion 3 ni muhimu kwani umeme 2100vutaendesha viwanda vyetu.
-mil 1 hadi mil 2 wameandikishwa kusoma bure, kwangu mimi ninaliona ni zuri kuliko hizi bil 23 kila mwezi kujiongezea mishahara.
-Kwangu mimi naona hizi hela ni bora kuziweka kwenye miradi kuliko kujiongezea mishahara. Mkitaka hii miradi yote tulioianzisha tuifute ili tujipandishie mishahara mimi sina tatizo hata kujilipa mil mbilimbili. Kupanga ni kuchagua.
-Tukitekeleza hii miradi yote haitachukua muda mrefu mishahara yetu bila kuiongeza na hii si lazima mei mosi.
-Ningekuwa na hela kwenye chungu zimebaki pale leo ningetamka tu. lakini nikitamka ntazitoa wapi? Nina mpango wa kuajiri wafanyakazi 52 elfu, ntawalipa nini? Dhamira yangu inanituma kwamba kusubiri ni kitu kizuri. Hebu tujenge miundo mbinu na kuajiri hawa 52,000/.
-Kwa hali ya sasa ni lazima niwaeleze ukweli. Tutaendelea kulipa viporo vya madeni.
-Mwaka huu nitaongeza nyongeza ya mshahara ya kila mwaka
-Kutakuwa na mifuko mili, mmoja wa watumishi wa umma na mwimgine kwa watumishi binafsi.
-Hii italahisisha kulipa mafao. Mifuko ilikuwa inashindana wenyewe kwa wenyewe.
-Katika kipindi hiki deni la tril 1.4 tumelipa katika mifuko ya pensheni. Kaeni ili mifuko hii miwili ianze kufanya kazi.
-Kuhusu haya Maswala ya masirahi ya wafanayakazikimsingi yanategemea kiwango cha kipato. Ndama hunyonya kiwango cha maziwa aliyonayo Mama yake.
-Nimeteua Majaji ambao watapunguza kesi kwenye mahakama ya kazi.
-Sijasema kila mfanyakazi awe amemaliza kidato cha nne bali kila mtu afanye kazi sehemu inayoendana na elimu yake.
-Hatupati watalii wengi kwasababu tulikuwa hatuna usafiri wa anga. tumeanza kulifanyia kazi.
Mkakati wa kutangaza Vivutio kama Ruaha, Kitulo maua ndwele, Kalambo ya Pili afrika Karenga na Isimili nk yanaendelea.
-Tumeamua kununua ndege saba na tatu zimeshawasili na nyingine nne zinawasili hapo baadae mwaka huu zikiwemo ndege kubwa mbili. Hii itaimalisha utalii.
-Mumeshauri kuimalisha sekta ya Elimu. Swala la elimu ni agenda ya serikali ya awamu ya tano. Hili tumeshaanza kulifanyia kazi. Kwenye elimu tumesambaza vifaa vya maabara na kuajiri walimu na tumefunga vyuo visivyo na sifa.
-Tumepanga kupeleka umeme kwenye vijiji vyote 176 kwenye Mkoa huu. Tumekamilisha hospitali ya Iringa Manispaa, Tutafanyia kazi eneo la Hospitali linaloingiliana na Magereza. Hii Hospitali ni Muhimu sana kwa watu wanaotoka Cairo hadi Afrika kusini wataitumia sana
-Ntaenda kuweka jiwe la Msingi hospita ya Kiroro.
-Tumetenga pesa za kujenga barabara kutoka Iringa hadi Msembe Kilometa 104
-Kwenye Mkoa huu hamlipishwi kodi ya mazao chini ya tani moja, wakina mama machinga tunawatengeneza vitambulisho ili msisumbuliwe.
-Nawahakikishia wafanyakazi wote serikali yenu inawathamini wala siwezi nikawashahu. Najua mnayoyafanya ayanleta tija. Naomba muamini leo. Msigwa ananichomekea moshi nliahidi. Sikuahidi leo ndo ninaweza kuahidi.
-Naomba niahidi na mniquote kweli kweli “Kama miradi hii itamalizika vizuri, kama tukiajiri watu elfu hamsini nambilia kuwalipa vizuri, kipindi changu cha urais hakitaisha kabla ya kupandisha mishahara ya wafanayakazi”. Kupandisha kwangu hakutakuwa kwa elfu kumi bali kutakuwa kuapndisha kweli kweli. Naomba muiamini Serikali yenu.
-Nachotaka kuwambia ndugu zangu, nawapenda wafanyakazi. Nlitamani mwaka huu kupandisha, lakini baada ya kuona hizi changamoto tulizonazo nikaona tuzimalize kwanza na kucontrol bei ya bidhaa. Naomba mnielewe ndugu zangu wafanyakazi
-Nyuso za upendo mlizonionyesha leo zimenigusa sana. Nyinyi ni watoto wa wakulima na wafugaji, nimewafutia tozo zaidi ya 87, ni jambo zuri sana.
-Nawashukuru vyama vyote vya wafanyakazi kwa maandalizi Mazuri. Nawashukuru sana Wanairinga. Na juzi nlipokelewa na WanaCCM nikajua CCM haijafa Iringa kulikuwa na uongozi mbaya tu. Leo Tungepiga kura hata kama ni Mahiga leo angeshinda Vizuri sana. Wanairinga hawakujua huyu ni wa Muhimu. Mlipomkataa mimi nikamchukua akawa mbunge na Waziri. Anafanya kazi nzuri sana.
-Siwezi kuisahau iringa, nakumbuka tulikuwa tunaenda pale stand kwa Mbata kusikiliza disco na mengine mengi. Sijui kama bado upo.
Mkoa wa Iringa umeshika nafasi ya Pili kwa ugonjwa wa Ukimwi inayoongoza ni Njombe 11%, Iringa maambukizi ni 11.2% katika watu 100 watu 12.2 ni Wagonjwa.
Zamani wanairinga walikuwa wanasema “Ukiona nimenyamasa ngusa tu sambi sako mwenyewe|”. Sasa hivi ukiangusha ujue kuna ukimwi.
Nawashukuru Wana Iringa, Sijawahi kupata makaribisho makubwa namna hii hapa Iringa. Nina deni kubwa, na naomba Mawaziri wanikumbushe katika madeni ya iringa ili niyamalize haraka. Sitawaangusha.
Wafanyakazi nawashukuru tena. Tanzania ina changamoto nyingi. tuirinde amani yetu tuuulinde mshikamano wetu. Tusibaguane kwa vyama vyetu, Ndo Mbunge Msigwa kaenda kukaa katikatika ya Wanaccm ili anukie vizuri.
Najua baada ya hapa kila mtu ataenda kuongea anayoyajua yeye, ila nawaomba waandishi wa habari waje niwape haya nliyoyasema na kuzungumza ili wasije wakapotosha.
Kuna mama amejitokeza akilia, anasema anaitwa Salima Koli anasemea alishambuliwa mwaka jana na kuuliwa kiumbe chake tumboni na kuharibiwa kizazi. “Mimi hapa nina familia na nina watoto. Nalalamika Mahakama haijanitendea haki. Nilishambuliwa na kijana mmoja. Nmekosa haki ya Kisheria”.
Rais amemuagiza RPC na mkuu wa Mkoa kwenda kwa mama Kuchukua jina lake na kumsikiliza kisha watampa mrejesho. rais amesema “Yule aliyempiga hata kama alishinda mahakamani, mkamateni mwende kumshitaki tena. Mchunguzeni huyo mama pia kama Kizazi chake kimetolewa”. Nawashukuru sana.