×

Rais Magufuli Ataka Mama Huyu Apimwe Kizazi – Video

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa Iringa na Kamanda wa Polisi mkoani humo kumpatia msaada mwanamama Salmakoni Sanga na kumpima iwapo ametolewa kizazi baada ya kudai kushambuliwa na kijana aliyemtaja kwa jina moja la Mussa.

 

Magufuli ametoa agizo hilo leo MEI 1, 2018 wakati akimaliza kuhutubia katika Sherehe za Siku ya Wafanyakazi ‘Mei Mosi’ ambapo Kitaifa zimefanyika katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa kufuatia mama huyo alijitokeza na kumlilia Rais ampatie msaada kutokana na kunyimwa haki yake mahakamani.

 

Mama Sanga amesema tukio lake la kushambuliwa na Mussa lilimtokea mwaka jana huku shambulio hilo likimfanya apoteze kiumbe alichokuwa nacho tumboni hali iliyompelekea kutolewa kizazi.

 

Aidha, mama huyo amedai licha ya maumivu aliyosababishiwa na kijana huyo, mahakama ilimuachia huru mtuhumiwa huyo huku yeye akiamini kwamba alidhulumiwa haki yake na mahakama ya mkoa huo.

 

Akitoa maagizo, Rais Magufuli amemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire na Mkuu wa Mkoa, Amina Masenza kumtafuta kijana huyo na kumfungulia mashtaka upya hata kama alishinda kesi.

Rais Magufuli Ataka Mama Huyu Apimwe Kizazi – Video