Msanii Mkongwe wa filamu nchini, King Majuto, amesafiri leo kuelekea India kwa ajili ya matibabu kutokana na ugonjwa wa Nyonga unaomsumbua kwa muda kidogo.
Baadhi ya wasanii mbalimbali nchini akiwemo, Duma, Nuh Mziwanda, Mzee Hashim Kambi, wamejitokeza katika uwanja wa ndege wa Mwil Julius Nyerere, kumsindikiza nguli huyo.