
LICHA ya kuwa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ inasifika kwa kuwa na wachezaji wengi mastaa wanaolipwa mishahara mikubwa mfano Paul Pogba na Alexis Sanchez lakini bado imekuwa ngumu kutamba katika orodha ya wanaofunika kwa mkwanja.
Kuna baadhi ya mataifa ambayo pia yamekuwa yakilipa mishahara mikubwa kwa wachezaji hasa wanaoelekea kustaafu kutoka Ulaya ili kuzifanya ligi zao ziwe na mvuto, lakini bado wale wa Ulaya wamekuwa wakilipwa vizuri kwa jumla kuliko wengine.

Mbali na mishahara, fedha nyingi wachezaji wamekuwa wakilipwa katika posho na matangazo ya kibiashara ambayo ni ya kwao binafsi pamoja na yale ya klabu zao.
Kuna makocha ambao nao wamekuwa wakilipwa vizuri anayeongoza ni bosi wa Manchester United, Jose Mourinho wakati ambapo mpinzani wake kwa ukaribu, Pep Guardiola wa Manchester City anashika nafasi ya tano.
Guardiola yupo nyuma ya Marcello Lippi, Diego Simeone na Zinedine Zidane.
Kutokana na utafiti uliofanywa huko nchini Ufaransa, hawa ndiyo wachezaji 10 wanaoongoza kwa malipo mazuri kwa kujumlisha fedha zote wanazolipwa kwa mwaka mmoja uliopita:

- Manuel Neuer
Klabu: Bayern Munich
Pauni 18.2m (Sh bilioni 57)
Licha ya kuwa alikuwa nje ya uwanja muda mrefu kutokana kuwa majeruhi, malipo yake yaliendelea kuwa vilevile kwa kuwa tu mikataba aliyosaini tangu mwanzoni mwa msimu ilikuwa haijavunjwa.

- Paul Pogba Manchester United Pauni 19.2m (Sh bilioni 60)
Licha ya kuwa bado kumekuwa na hoja kadhaa juu ya hatima yake lakini hiyo haijaondoa ukubwa wa jina lake na jinsi ambavyo amekuwa akijiingizia fedha. Bado yupo kikosi cha kwanza na hiyo imemsaidia kumuongezea umaarufu.
- Robert Lewand-owski Bayern Munich Pauni 19.4m (Sh bilioni 60.5)
Ni kinara wa mabao katika Bundesliga, anatajwa kuwa anaweza kwenda Real Madrid lakini hilo bado halijathi-bitishwa. Siyo mzungu-mzaji sana lakini yumo kwenye orodha.
- Oscar Shanghai SIPG Pauni 19.4m
Aliamua kuondoka Chelsea kufuata fedha, anaingia katika orodha hii kwa kuwa ana malipo mazuri ya mshahara akiwa anacheza soka nchini China. Alitua huko kusaidia kukuza ligi ya nchi hiyo.
- Edinson Cavani Paris Saint-Germain Pauni 19.7m (Sh bilioni 61.5)
Ndiye mfungaji mwenye rekodi ya kipekee katika timu hiyo, akiwa ndiye anayeongoza kwa mabao kwa jumla, hajaonyesha dalili za kupunguza kasi na ndiyo maana imechangia kupata mkwanja mwingi kutoka kwa matajiri wa Kiarabu wanaoimiliki timu hiyo.
- Thomas Muller, Bayern Munich, Pauni 20.1m (Sh bili-oni 63)
Mshambuliaji mkongwe wa Bayern ambaye taratibu umri unaanza kumuacha, kasi yake imepungua lakini bado heshima yake haijapungua na ukubwa wa jina lake umemfanya aendelee kulipwa mpunga mrefu.
- Karim Benzema
Real Madrid
Pauni 20.6m (Sh bilioni 64)
Ameshindwa kuwa na kasi kubwa ya kufunga mabao msimu huu kiasi cha kuanza kuhususishwa kuwa ataondolewa klabuni, akiwa kwenye ubora wake alifaidika kupata mikataba minono ambayo ndiyo imemfanya aendelee kutamba hadi sasa.
- Alexis Sanchez
Manchester United
Pauni 20.6m (Sh bilioni 64)
Usajili wake wa Januari kutoka Arsenal umemuongezea thamani mchezaji huyo ambapo sasa anakuwa juu ya Pogba aliyekuwa akitamba kikosini hapo kwa malipo mazuri. Wawili hao ndiyo pekee kutoka Premier League waliongia katika orodha hii.
- Ezequiel Lavezzi
Hebei China Fortune
Pauni 22.1m (Sh bilioni 69)
Huyu aliamua kuondoka mapema Ulaya na kwenda China kuboresha akaunti yake ya benki, kweli hilo liliwezekana na ndiyo maana licha ya kutokuwa na ustaa kama wengine kadhaa wa Ulaya lakini bado amemudu katika nafasi hii.
11) Andres Iniesta
Barcelona
Pauni 22.3m (Sh bilioni 70)
Wiki kadhaa baadaye ataondoka klabuni hapo kwa kuwa ameshat-angaza kuwa anaelekea nje ya Ulaya kumalizia maisha yake ya soka, hilo halijazuia kuwemo katika orodha hii kwa kile ambacho alikipata mwaka mmoja uliopita.
10) Luis Suarez
Barcelona
Pauni 22.7m (Sh bilioni 71)
Staa mwingine wa mabingwa hawa wa Ligi Kuu ya Hispania msimu huu, anaingia kutokana na ubora wa kazi yake uwanjani, amefunga mabao mfululizo tangu atue akitokea Liverpool.
- Antoine Griezmann
Atletico Madrid
Pauni 22.7m (Sh bilioni 71)
Haijajulikana juu ya majaaliwa yake kwa kuwa anahusishwa kwenda Barcelona, hiyo inatokana na uwezo wake wa kufunga na ndiyo maana ni tegemeo la Ufaransa na klabuni.
- Zlatan Ibrahi-movic
LA Galaxy
Pauni 23.4m (Sh bilioni 73)
Kama angeendeelea kubaki Manchester United angekuwa mchezaji wa tatu kwa wanaolipwa vizuri klabuni hapo, kuondoka kwake kumemfanya aendelee kuingia kwenye orodha hii kwa kuwa hata akiwa Marekani pia analipwa vizuri. Malipo yake mengi ameyapata kutokana na matangazo ya biashara.
- Sergio Ramos
Real Madrid
Pauni 24.1m (Sh bilioni 75)
Mmoja wa wachezaji raia wa Hispania watatu waliomo katika orodha hii, ubora wake kwa misimu kadhaa umechangia kumfanya awe analipwa mshahara mkubwa kuliko mabeki wengi.
- Toni Kroos
Real Madrid
Pauni 24.7m (Sh bilioni 77)
Ndiye Mjerumani anayelipwa vizuri kwa jumla kuliko wote katika mataifa yote, na hiyo ni kwa kuwa yupo katika klabu tajiri ambayo suala la fedha kwao ni kitu cha kawaida kutumia.
- Gerard Pique
Barcelona
Pauni 25.4m (Sh bilioni 79)
Beki anayelipwa vizuri kuliko wote duniani, ndiye Mhispania wa watatu katika orodha hii baada ya Ramos na Iniesta. Analipwa vizuri kutokana na ubora wake uwanjani na pia anaelekea kuwa kiongozi wa timu hiyo miaka kadhaa ijayo, hilo ndilo lengo lake.
- Gareth Bale
Real Madrid
Pauni 38.5m (Sh bilioni 120)
Alisajiliwa huku Madrid wakiwa na matarajio makubwa kutoka kwake lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo, ubora wake haujafikia pale ambapo wengi waliteg-emea huku majeraha yakimuandama, uzuri ni kuwa tayari alishapata mikataba mapema.
- Neymar
Paris Saint-Germain
Pauni 71.3m (Sh bilioni 223)
Wale waliokuwa wakijuliza kwa nini alikubali kuihama klabu kubwa kama Barcelona, inawezekana alitaka kuondoka kwenye kivuli cha Lionel Messi lakini upande wa pili kulikuwa na fungu kubwa la fedha lililotumika kumshawishi atue Ufaransa.
Analipwa mshahara mnono, nje ya hapo kuna fedha nyingi anaingiza kutokana na malipo ya matangazo ya jina na taswira yake, ndiye mchezaji aliyesajiliwa kwa dau kubwa zaidi kuliko wote duniani. Pauni 198 (Sh bilioni 618) zilitumika kumhamisha.
- Cristiano Ronaldo
Real Madrid
Pauni 82.2m (Sh bilioni 257)
Mreno ambaye anajua kuzitafuta kwa nguvu, anapewa ushindani mkali na Messi uwanjani lakini mara zaote amekuwa akipambana kuhakikisha naye anakuwa bora japokuwa kuna wakati mambo hayaendi sawa.
Analipwa takribani mara mbili ya kile ambacho Bale analipwa lakini yote hiyo ni kwa kuwa juhudi zake uwanjani ni kubwa na dunia yote inaona hilo.
- Lionel Messi
Barcelona
Pauni 110.2m (Sh bilioni 344)
Messi na Ronaldo wamekuwa na ushindani katika sehemu nyingi, baada ya Ronaldo kuongoza kipindi fulani, mpinzani wake huyu aliboreshewa mkataba na ndipo akampiga bao.
Kiwango anacholipwa ni kikubwa na kimemuacha mbali Ronaldo, mkataba wa Messi ulioboreshwa ni mnono na mrefu ambao Ronaldo anatakiwa kufanya kazi kubwa kuupiku.